Sensei yahya Omar Mgeni ni miongoni mwa waalimu wachache hapa
nchini Tanzania wenye sifa kima zake, ni mwalimu mwenye kujitolea katika
kueneza mchezo wa karate na misingi yake yaDOJO-KUN na NIJU-KUN ni mwalimu pekee anayefundisha karate kama BUDO,
ni mwenye kushirikiana na waalimu mbalimbali.
Anashaurika,
mzalendo na amekuwa ni chachu ya kuzaliwa kwa chama cha karate Shotokan
"TASHOKA" (Tanzania ShotokanKarate) pia
kuzaliwa kwa T.K.F (Tanzania Karate Federation).
Ameanza safari ya kujifunza Shotokan Karate mnamo
mwaka 1986 chini ya kocha Sensei Mustafa Ahmed nchini Kenya, mpaka mwaka 1989
akiwa na 1st kyu Brown Belt, kisha alipata
Scholarship kwenda Egypt ambako alijiunga na
klabu ya polisi “NAD-EL-SHURTA” iliyoko Abbasiya Cairo, hapo aliendelea
kujifunza chini ya kocha wa timu ya taifa ya Egypt wakati ule sensei kapteni
Zakaria, Mnamo mwaka 1993 alifanya grading ya Sho-dan iliyosimamiwa na E.K.F
(Egypt Karate Federation).
Mnamo mwaka 1994 alishiriki semina ya urefa
iliyosimamiwa na E.K.F iliyofanyika Alexandria na mwaka 1995 alishiriki semina
ya urefa iliyosimamiwa na E.K.F iliyofanyika Port Said.
Ameshiriki tournament nyingi za vilabu na vyuo
nchini Egypt na kuchukua medali na vikombe. Mwaka 1996 alirejea nchini
na kuasisi klabu ya Karate “Iringa Karate Shotokan Club” kutokana na
kutokuwepo na vilabu vinavyozielewa sharia za W.K.F wakati ule alilazimika
kwenda Kenya kuomba ushiriki wa mashindano mbalimbali huko.
Mnamo mwaka 1999 alipeleka timu ya mkoa wa Iringa
kushiriki mashindano ya vilabu- interclub (Coast championship) timu ya Iringa
ilifika robo fainali baada ya kutolewa na timu ya (Navy). Mnamo mwaka 2000
alipeleka timu Mombasa Kenya ya watoto under 15 na kurudi na medali ya dhahabu.
Mnamo mwaka huu Sensei Yahya O Mgeni alifanya grading Ni-dan iliyosimamiwa na
Coast Karate Association.
Mwaka 2002 Iringa ilipokea timu toka Kenya na
kucheza nayo Friendly match na mwaka 2003 Iringa ilipokea timu tena toka Kenya
na kucheza nayo. Mwaka 2005 Sensei Yahya O Mgeni alihama Iringa na kuhamia Dar
es salaam na kuasisi “Serengeti Shotokan Karate Club” Mwaka 2006, mnamo mwaka
2007 Iringa ilishiriki “Sababa Tournament” iliyoandaliwa na ubalozi wa Japan
chini ya usimamizi wa mkufunzi kutoka Japan Sensei Yushi Fuji na kutoa ushindi,
Mnamo mwaka 2008 Serengeti ilipata mwaliko wa shindano la karate “Japan Karate
Championship” team na individual lililofanyika Don-bosco chini ya usimamizi wa
Shihan Mishaly toka South Africa, Serengeti ilikuwa mshindi wa kwanza timu na
individual (mshindi wa kwanza na wa pili).
Mnamo mwaka 2009 ubalozi wa Japan uliandaa
shindano lililosimamiwa na Sensei Kaneto, Serengeti Shotokan ilichukua nafasi
ya kwanza kumite na kata.
Mnamo mwaka 2012 Sensei Yahya O. Mgeni alipeleka
timu ya Tanzania kushiriki mashindano ya dunia “World Karate Tournament”
yaliyofanyika Malindi Kenya na kushirikisha Zaidi ya nchi kum. Mwaka huu
Serengeti ilihudhuria Semina ya kimataifa ya Karate iliyosimamiwa na Shihan
Farid Al-shuhaiby Chief instructor ISKF Oman iliyofanyika Zanzibar.
Mnamo mwaka 2013 kwa juhudi zake Sensei Yahya
alifanikiwa kupata uanachama wa shirikisho la Karate I.S.K.F- International
Shotokan Karate Federation lenye makao yake makuu marekani chini ya Shihan
TERIYUKI OKAZAKI SENSEI 10TH DAN na mnamo mwaka huo Sensei Yahya O. Mgeni
alifanya grading ya kimataifa ya San- dan chini ya Shihan Farid Al-shuhaiby 7th
Dan na walifanya wanafunzi wake Sho-dan , Ni-dan, na San-dan.
Hadi sasa Sensei Yahya O. Mgeni ndiye sensei
mwenye wanafunzi wengi Tanzania, anao black belt 50 na kyu ranks 200 na ni
sensei wa kwanza mwenye vilabu vingi Tanzania.

